Ad Code

PART 4. KWANINI MUNGU ALITUUMBA?

 PART 4.


SOMO:KWA NINI MUNGU ALITUUMBA? 

       2.MUNGU ALITUUMBA ILI TUMTUMIKIE. 

-Tunaendelea pale tulipoishia, wote tumeagizwa kumtumikia Mungu (Zaburi 72:11 ; Zaburi 22:30 ; Mathayo 28:18-20 ;

                  Mathayo 16:15-16) 

*11 Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie. 

Zaburi 72:11

* 30 Wazao wake watamtumikia. Zitasimuliwa habari za Bwana, Kwa kizazi kitakachokuja, 

Zaburi 22:30

* 18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 

Mathayo 28:18

19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 

Mathayo 28:19

20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. 

Mathayo 28:20

* 15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 

Marko 16:15

16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. 

Marko 16:16

      -> Agizo kuu hili linatuhusu wote na si baadhi

[13/08 10:13] MWAMBUBA: **Tutatumikaje sasa?  - Kumtumikia Mungu si kuhubiri peke yake, kuna namna nyingi za kumtumikia Mungu, vipawa ni tofauti na karama pamoja na huduma nitofauti kila mtu atumike sawasawa na alivyopewa kutumika si kwa kuigana. 

                             (   1Wakorintho12:4-7,Efeso 4:11-12)

         4 Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. 

1 Wakorintho 12:4

5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. 

1 Wakorintho 12:5

6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. 

1 Wakorintho 12:6

7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. 1 Wakorintho 12:7

          11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 

Waefeso 4:11

12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; 

Waefeso 4:12

       - >Kwanini vipawa/karama na huduma tofauti? Ni ili kazi ya Kristo itendeke kwa ubora na

[13/08 10:14] MWAMBUBA: ubora na mwili wa Kristo ujengwe, na si kwa ajili ya mashindano. 

      - >Kumtumikia Mungu kunahitaji unyenyekevu, utii, unyenyekevu si kuwa ndio kwa kila kitu kwa maoni ya watu. 

     - >Yesu mwenyewe alitumika (Luka22:26-30; Marko10:45)

   45 Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi. 

Marko 10:45

     - >Kumtumikia Mungu kunahitaji bidii ya kimaksudi kabisa

                     (Rumi12:11)

   11 kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; 

Warumi 12:11

          @*USIPOMJUA MUNGU WA KWELI UTAJIKUTA

      UNATUMIKIA VITU VINGINE(MIUNGU ISIYOKUUMBA) @*

                (Galatia4:8)

      6 Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine. 

Wagalatia 1:6

7 Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. 

Wagalatia 1:7

8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili

[13/08 10:16] MWAMBUBA: yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. 

Wagalatia 1:8

9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe. 

Wagalatia 1:9 


       @Sasa ngoja niorodheshe namna mbalimbali za kuweza kumtumikia Mungu kama ifuatavyo;-


 A. KWA KUFANYA HUDUMA MBALIMBALI

  - Kwa kuhubiri injili, kulitangaza Neno la Mungu na

      kufundisha (1Timotheo4:11-16)

 - Kushuhudia watu, kuwaalika watu kanisani,nyumba kwa

      nyumba. 

 - Kuombea wengine-kufanya maombi na maombezi, watu

     waokolewe, waponywe, kuombea watendakazi wa injili

            (waefeso 6:18 ; Mathayo 17:21)

 - Kusaidia maono ya Mchungaji kutimia, kusimama na

      Mchungaji (Mathayo 10:41)

 - Uimbaji, uinjilisti kwa ujumla. 

 - Waangaliao utaratibu wa kanisa, watu wa itifaki,

       mashemasi, wazee wa kanisa. 

 B. KWA KUSAIDIA JAMII YENYE UHITAJI

 - Kuwatembelea Yatima na Wajane-kuwatia moyo, kuwafariji

      Kuwaombea, kuwasaidia kimahitaji

[13/08 10:19] MWAMBUBA: kwa hali na mali 

            (Yakobo1:27; Mithali 19:17)

 - Kusaidia maskini na wasiojiweza (Walemavu) 

           (Kumbukumbu15:11;Mithali 14:21,31)

 - kutembelea wagonjwa na waliodhaifu kwa maombi na mali

           (Zaburi 41:1-3)

 C.KUJITOA KWA KUFANYA KAZI YA MIKONO KANISANI

       - Kufanya usafi mfano, kufagia, kudeki, kufyeka,   

    Kubeba vyombo(speakers) hakuhitaji roho, msemo wa

     "tuko pamoja kiroho mtumishi" hauhitajiki

    hapa - tuitoe miili yetu kwa kazi pia( Warumi12:1)

D. KUTUMIKA KWA MALI ZAKO KANISANI (Mithali 3:9-10)

        ¡) Kutoa sadaka (Malaki 1:6-8,11-14)

       ¡¡) Kulipa Zaka (Malaki 3:8-10)

      ¡¡¡) Kutoa vitu vinginevyo(Mali mbalimbali) (Mithali 11:25)

             - Magari, nyumba, viwanja, pesa, vyombo mbalimbali

                 ili kupeleka injili (Warumi10:11-15)


       %Tutaendelea Asanteni sana, Mungu atubariki sote%

               BY MWAMBUBA,  #SAUTI YA MJUMBE#

Chapisha Maoni

0 Maoni

Close Menu