Ad Code

PART 3 SOMO:KWA MUUNGU ALITUUMBA? 2.MUNGU ALITUUMBA . KUTOKA 23:25a 25 Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. Kutoka 23:25 - Kutumika ni kitendo cha kumfanyia kazi mtu au serikali au ufalme fulani kwa makubaliano ya malipo ya kiasi fulani. -Kuna utofauti kati ya kutumika na kutumikishwa, kutumikishwa hakuna tofauti sana na utumwa yaani unamtumikia mtu kwa faida yake, anaweza akulipe kidogo ama asikulipe kabisa. -Mungu alimuumba mtu duniani si ili amwabudu tu baliamtumikie pia na hii ndio maana tunapookoka hatuendi mbinguni tunabaki hapa duniani ili kumtumikia Mungu. -Kimsingi tupo hapa duniani kwaajiri ya wengine. Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. Wafilipi 1:21 *Mungu wetu anataka tumtumikie tena kwa furaha. Zaburi 100:2. 2 Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba; Zaburi 100:2 -Mungu anataka watu wake wamtumikie Yeye Kutoka 8:1,20, 1Samweli 12:24 -Hapo awali Mungu alichagua Taifa moja ili limtumikie Mungu (Israel) na waweze kuangusha na kuibomoa kabisa miungu yoyote mbele yao, ona jinsi ilivyo serious hili jambo... Kutoka 23:24,33 ; Kumbukumbu 5:9 ; 7:16 16 Nawe angamiza mataifa yote atakayokupa Bwana, Mungu wako; jicho lako lisiwahurumie, wala usiitumikie miungu yao; kwani litakuwa ni mtego kwako jambo hilo. Kumbukumbu la Torati 7:16 - Kwa hiyo ili umtumikie Mungu vizuri na kwa mafanikio ni lazima baadhi ya mambo yasiompendeza Mungu yafe hata kama bado unayahitaji au unayapenda. - Kujua hayo mambo ni rahisi tu, mfano unataka kuomba, je ni jambo gani linakunyima muda wa kuomba? Lifutilie mbali. Unaona ugumu wa kuhubiri injili, kutoa, kujitoa kwa kazi za mikono kanisani, futa kwanza kizuizi, cha weza kuwa ni simu yako, mali zako, cheo chako, ndoa yako n.k, nadhani hekima ya Ki Mungu itumike sana kwenye baadhi ya maeneo nimetaja. Ila kazi ya Mungu lazima isonge mbele na amani ya familiya yako idumu. Huwezi tumikia mabwana wawili wenye hadhi sawa utachanganyikiwa, lazima Yesu awe kipaumbele cha kwanza kuliko vyote. * Ili umtumikie Mungu kwa faida nilazima ufate vigezo :- - Yalikuwepo mavazi maalumu kwa ajili ya watumishi wa Mungu. 19 na mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, kwa ajili ya kutumika ndani ya mahali patakatifu, hayo mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani. Kutoka 35:19 ; Kutoka 31:10 - Huwezi kumtumikia Mungu kwa faida bila kuokoka(kumvaa Kristo Yesu) maana ili ukubaliwe na Mungu lazima umpokee Yesu kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yako binafsi. - Kwenye agano jipya sisi sote ni makuhani watakatifu tumeitwa tumtumikie Muumba wetu, na si wote ni wale tu waliompokea Yesu, basi kama kuna mtu anadai anamtumikia Mungu bila kumpokea Yesu(kuokoka) anajipendekeza na kupoteza muda, hajulikani na Mungu. Njia ni Yesu pekee(Yohana 14:6,Yohana 1:12). 9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; 1 Petro 2:9 10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema. 1 Petro 2:10 - Wote tunapaswa tumtumikie aliyetuumba ila kigezo ni wokovu kupita Mwanaye Yesu Kristo nje na hapo utatumikiswa kwa faida ya ufalme bila wewe kunufaika maana mwishowe utakataliwa.Sema, Hili jambo liniepuke. 11 Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie. Zaburi 72:11 30 Wazao wake watamtumikia. Zitasimuliwa habari za Bwana, Kwa kizazi kitakachokuja, Zaburi 22:30 13 Mche Bwana, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake. Kumbukumbu la Torati 6:13 *TUTAMTUMIKIAJE MUNGU?....... TUTAENDELEA....

 

PART 3
SOMO:KWA  MUUNGU ALITUUMBA? 
2.MUNGU ALITUUMBA ILI TUMTUMIKIE
                KUTOKA 23:25a

25 Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia  chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. 
Kutoka 23:25

- Kutumika ni kitendo cha kumfanyia kazi mtu au serikali au ufalme fulani kwa makubaliano ya malipo ya kiasi fulani. 
-Kuna utofauti kati ya kutumika na kutumikishwa, kutumikishwa hakuna tofauti sana na utumwa yaani unamtumikia mtu kwa faida yake, anaweza akulipe kidogo ama asikulipe kabisa. 
-Mungu alimuumba mtu duniani si ili amwabudu tu baliamtumikie pia na hii ndio maana tunapookoka hatuendi mbinguni tunabaki hapa duniani ili kumtumikia Mungu. 
-Kimsingi tupo hapa duniani kwaajiri ya wengine. 

Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.
Wafilipi 1:21
   
     *Mungu wetu anataka tumtumikie tena kwa furaha.        Zaburi 100:2. 
    2 Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba;
Zaburi 100:2
-Mungu anataka watu wake wamtumikie Yeye
      Kutoka 8:1,20,  1Samweli 12:24

-Hapo awali Mungu alichagua Taifa moja ili limtumikie Mungu (Israel) na waweze kuangusha na kuibomoa kabisa miungu yoyote mbele yao, ona jinsi ilivyo serious hili jambo... 
Kutoka 23:24,33 ; Kumbukumbu 5:9 ; 7:16

16 Nawe angamiza mataifa yote atakayokupa Bwana, Mungu wako; jicho lako lisiwahurumie, wala usiitumikie miungu yao; kwani litakuwa ni mtego kwako jambo hilo. 
Kumbukumbu la Torati 7:16
  - Kwa hiyo ili umtumikie Mungu vizuri na kwa mafanikio ni lazima baadhi ya mambo yasiompendeza Mungu yafe hata kama bado unayahitaji au unayapenda. 
  - Kujua hayo mambo ni rahisi tu, mfano unataka kuomba, je ni jambo gani linakunyima muda wa kuomba? Lifutilie mbali. 
Unaona ugumu wa kuhubiri injili, kutoa, kujitoa kwa kazi za mikono kanisani, futa kwanza kizuizi, cha weza kuwa ni simu yako, mali zako, cheo chako, ndoa yako n.k, nadhani hekima ya Ki Mungu itumike sana kwenye baadhi ya maeneo nimetaja. Ila kazi ya Mungu lazima isonge mbele na amani ya familiya yako idumu. Huwezi tumikia mabwana wawili wenye hadhi sawa utachanganyikiwa, lazima Yesu awe kipaumbele cha kwanza kuliko vyote. 
   * Ili umtumikie Mungu kwa faida nilazima ufate vigezo :-
     - Yalikuwepo mavazi maalumu kwa ajili ya watumishi wa Mungu.  
     19 na mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, kwa ajili ya kutumika ndani ya mahali patakatifu, hayo mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani.
Kutoka 35:19 ; Kutoka 31:10
     - Huwezi kumtumikia Mungu kwa faida bila kuokoka(kumvaa Kristo Yesu) maana ili ukubaliwe na Mungu lazima umpokee Yesu kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yako binafsi. 
    - Kwenye agano jipya sisi sote ni makuhani watakatifu tumeitwa tumtumikie Muumba wetu, na si wote ni wale tu waliompokea Yesu, basi kama kuna mtu anadai anamtumikia Mungu bila kumpokea Yesu(kuokoka) anajipendekeza na kupoteza muda, hajulikani na Mungu. Njia ni Yesu pekee(Yohana 14:6,Yohana 1:12). 

      9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; 
1 Petro 2:9
10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema. 
1 Petro 2:10
   - Wote tunapaswa tumtumikie aliyetuumba ila kigezo ni wokovu kupita Mwanaye Yesu Kristo nje na hapo utatumikiswa kwa faida ya ufalme bila wewe kunufaika maana mwishowe utakataliwa.Sema, Hili jambo liniepuke. 

       11 Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie. 
Zaburi 72:11
        30 Wazao wake watamtumikia. Zitasimuliwa habari za Bwana, Kwa kizazi kitakachokuja, 
Zaburi 22:30
       13 Mche Bwana, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake. 
Kumbukumbu la Torati 6:13
           *TUTAMTUMIKIAJE MUNGU?....... TUTAENDELEA.... 





        


       











Chapisha Maoni

0 Maoni

Close Menu