Ad Code

KWANINI MUNGU ALITUUMBA?


 SOMO:KWANINI MUNGU ALITUUMBA? 

                   ZABURI 100:3

                    ISAYA 43:10

UTANGULIZI

   - Kila kitu kilichopo duniani kuna sababu maalumu ya uwepo wake. 

   - Iwe kiumbe hai au kisichokuwa hai ili mradi kipo duniani uwepo wake una maana 

      maalumu na kazi nakusudi fulani muhimu. 

°Ngoja nitoe mfano wa vitu hivi viwili vilivyotengenezwa na wanadamu

   - kusudi l kutengeneza Redio ni ili watu wasikilize habari mbalimbali na si kuona, hivyo basi ukitaka kuona Kipo kifaa au chombo maalumu kwa kazi hiyo(TV) ukichanganya maada hapa utapata matokeo tofauti na ulio tarajia. 

  -  Kuna vitu viwili wingine nitolee mfano, Perfume ilitengenezwa maalumu kwa ajili ya kupulizia kwenye nguo ili ilete harufu nzuri kwa binadamu, hiyo ni nzuri ila hiyo harufu nzuri haifai kupuliza kwenye chakula ili kilete radha bali utatia Royco au Mchuzi mix ili chakula kilete radha fulani nzuri sana. Kadhalika mchuzi mix haifai kupaka kwenye nguo.Hahaha......... Utanielewa ukiendelea mbele. 

   - Kutokujua kwanini tuliumbwa tunajikuta tunachanganya mafaili, tunachanganya vitu, mambo, kifupi tunayakoroga na mbaya zaidi tunabadilishiwa matumizi. 

SWALI :-je, Mungu alituumba kwa matumizi gani? Je,hivi ni kweli kwamba Mungu aliamua kuumba mtu asiyena faida kwake? Bila shaka sababu zipo. 


¤Sasa kabla hatujaangalia sababu nne za kwanini tuliumbwa naomba kuchunguza mambo tunayotakiwa kuyajua Kuhusu muumbaji wetu kulingana na maandiko yetu makuu Zaburi 100:3 na Isaya43:10.


@ZABURI 100:3

3 Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake. 

Zaburi 100:3


  A. Lazima tujue kuwa BWANA ndiye Mungu, Yaani Yesu ni Mungu (Tito2:13)

            13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu,

                    Mungu mkuu na Mwokozi wetu; Tito 2:13


     - Sifa ya Mungu ni kuumba na si kutengeneza, Yesu aliumba (Yohana 1:1-3,14)

 1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 

Yohana 1:1

2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 

Yohana 1:2

3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. 

Yohana 1:3


14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. 

Yohana 1:14

      - Yesu ni Mungu.(wakolosai2:2)

2 ili wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo; 

Wakolosai 2:2

         NB:

            - YESU NI BWANA MWENYEWE - - Wafilipi2:11

11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba. 

Wafilipi 2:11

            %%-Hivyo Bwana ndiye Mungu (Zaburi100:3a) Daka hii. 


    B. Ni lazima tujue yeye ndiye aliyetuumba na si mwingine, (Mwanzo 1:26)

                 -Ametuumba kwa mfano na sura yake,kwanini? Tusonge mbele kidogo. 

26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. 

Mwanzo 1:26.

                - Ametuumba tufanane naye, kitabia, kimatendo, kuongea, kimaisha, kimienendo n.k...wakolosai3:10 na mathayo26:73,Aliumba mwanaume na mwanamke. Tena ametuumba sote na tu kazi ya Mikono yake (Malaki2:10),(Waefeso 2:10)


10 Je! Sisi sote hatuna Baba mmoja? Mungu aliyetuumba siye mmoja tu? Basi, mbona kila mmoja wetu anamtenda ndugu yake mambo ya hiana, tukilinajisi agano la baba zetu? 

Malaki 2:10


10 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo. 

Waefeso 2:10


-Na kama tu kazi ya mikono yake ni basi tupo kwa ajili ya matumizi ya fundi(mwenyekazi-Mungu)( Isaya29:16) -na huwa chombo hakiwezi bishana na fundi wake, lazima kifuate makusudi ya kutengenezwa kwake. 


      16 Ninyi mnapindua mambo; Je! Mfinyanzi ahesabiwe kuwa kama udongo; kitu kilichofinyangwa kimnene yeye aliyekifinyanga, Hakunifinyanga huyu; au kitu kilichoumbwa kimnene yeye aliyekiumba, Yeye hana ufahamu? 

Isaya 29:16


   C. Ni lazima tujue sisi ni watu wake-yaani tu mali yake(1wakorintho6:20)

         -Tulinunuliwa kwa thamani tu mali yake (1Wakorintho7:23)

         - lazima tujue Yeye ni Baba nasi tu wana wa kike na kiume, ni Mungu wetu na ni 

            Baba yetu (2Wakorintho6:18; Yohana 20:17,28)lazima tuwe na uhusiano mzuri

             naye. 

          NB:-

              - Aliye mali ya mtu yupo kwa ajili ya matumizi ya mtu huyo, ni mtu au mtoto

       muasi pekee ndiye hafati maagizo ya bosi wake au ya babaye, asomaye na

          afahamu.     


     D. Ni lazima tujue kuwa sisis ni kondoo wa malisho yake-Anatutunza, anatulisha. 

          -Yeye ndiye mchungaji mwema hakuna haja ya hofu ya maisha ukiwa nae. 

            (Yohana10:11,14) kila kitu chema twapata kwake, hatutumikishi bila faida. 

11 Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. 

Yohana 10:11

14 Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi; 

Yohana 10:14

           - Yeye ndiye mpaji wa kila hitaji letu (Wafilipi4:6,; Mathayo7:7)

6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 

Wafilipi 4:6


           - Ni lazima tujue kuwa yeye ndiye anatulisha nakutuchunga kila siku, hutuongoza

                 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; (Isaya 1:19) 


    19 na kwamba tukikubali na kutii tutakula mema ya nchi. (Isaya1:19)


@ISAYA43:10

10 Ninyi ni mashahidi wangu, asema Bwana, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine. 

Isaya 43:10


      E. Sisi tu mashahidi wake na wawakilishi wake hapa duniani, tu mabalozi na kazi ya mabalozi ni kuwakilisha ufalme uliomtuma, kwa lipi, namna gani? Tutaona mbele. 

(2wakorintho5:20; 1Wakorinththo4:1-2)  Matendo10:39;41)

      

      F. Ni lazima tumwamini Mungu aliyetuumba

            - Kwa Mungu kutomwamini ni sawa na kumdharau (Hesabu14:11) na ndio maana hamfurahii mtu mwenye kusitasita(Waebrania10:38; 11:6) ukisita unapotea. Amini Muumba wako. 


       G. Ni lazima tujue kuwa hakuna MUNGU isipokuwa Yeye BWANA. 

-Hakuumbwa, alikuwepo,, yupo na atakuweko, na wala hakuna mwingine wa kulingana naye. 


    Tutaendelea.... ...



Chapisha Maoni

0 Maoni

Close Menu