Ad Code

PART 2 :KWANINI MUNGU ALITUUMBA?


 


KWA NINI MUNGU ALITUUMBA? 
-TUNAENDELEA TULIPOISHIA........ 
*Baada ya kuona na kuyaangalia maandiko ya msingi wa somo letu, sasa ni muhimu tuendelee mbele  kuangalia sababu muhimu ambazo zilinfanya Mungu atuumbe:-

1.MUNGU ALITUUMBA ILI TUMWABUDU
      ----Zaburi 95:6-8----
-Kuabudu ni zaidi ya kuimba
-Kuabudu ni zaidi ya kuwa na sauti nzuri (vocal) 
-Kuabudu ni zaidi ya kukusanyika jumapili kusali
-Kuabudu ni zaidi ya mziki mzuri wa taratibu
-Kuabudu ni zaidi ya kuimba nyimbo za taratibu au polepole
-Tuabudu ni mfumo mzima wa maisha ya kila siku ya Mtu. 
-Kuabudu sio tukio ni mienendo, misemo, mambo yote yanayo mpa Mungu heshima na utukufu anaostahili. 
           Malaki 1:6 maandiko yanasema,,,,........ 
6 Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? Bwana wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani? 
Malaki 1:6
   - Hivyo kuabudu ni zaidi ya maneno tuu, imempasa Mungu aabudiwe katika roho na kweli kwa maana Mungu ni Roho,aabudiwe tokea ndani ya roho zetu, maneno na Matendo viendane, Mungu atusaidie sana kizazi chetu hiki, maana maneno mengi na kukata viuno kanisani kwa jina la kumsifu Mungu, baada ibaada ni mingine kabisa, hiyo sio maana halisi ya Ibaada,   
              Yohana 4:23-24
23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. 
24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. 
  - Mafarisayo walidhani kumwabudu Mungu ni kusujudu, kuinama mbele za Mungu, kupiga magoti na kumwimbia na kusema habari za Mungu pasipo kuhusisha mioyo yao yaani bila kumakinika na kile wanafanya ibadani (nia mbili) Yesu akawaita ni wanafiki na hawaendi popote wasipobadilika
                       Marko7:5-9
     5 Basi wale Mafarisayo na waandishi wakamwuliza, Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuyafuata mapokeo ya wazee, bali hula chakula kwa mikono najisi? 
6 Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami; 
7 Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu, 
8 Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu.
9 Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu. 
    - Walidhani kumwabudu Mungu ni matendo ya kimpokeo, kimwili pekee, mfano ukitenda dhambi ukikamatwa hiyo ni dhambi na unastahili kupewa adhabu, ila ukitenda dhambi hujakamatwa wewe ni msafi mbele za watu unaonekana mwabudu halisi na mtakatifu ila kwa Mungu wewe bado ni mdhambi na ni mnafiki sana viwango vya juu. 
      - Anayestahili kuabudiwa ni Mungu muumba peke yake, kama hukuumba mbingu na nchi huna hadhi ya kuabudiwa, unabaki kuwa sanamu, midoli, matoi na vitu vyote vilivyochingwa ni kazi ya mikono ya wanadamu havifai kuabudiwa-ni upungufu wa ufahamu wa kiwango cha juu sanaa kuabudu kitu umekitengeneza mwenyewe, hasemi hawezi kusogea mpaka umuhamishe, Mungu gani huyo sasa anategemea msaada wa mwanadamu hahaha, Shetani mwongo sana. 
Watu wamenye akili wanamjua Mungu wao na katu hawaabudu sanamu. Soma Zaburi 96:4-5
3 Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake. 
4 Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana. Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote. 
5 Maana miungu yote ya watu si kitu, Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu. 
Mfano, 
         *Daniel alikataa kuabudu miungu - Daniel6:7,10
         *Shadrack, Meshack, Abednego walikataa kuabudu
              sanamu, (Daniel 3:14-18)
    - Je, Mungu wako anastahili kuabudiwa? Na kama anastahili ana kigezo cha  uumbaji? Yesu anaabudiwa maana aliumba kabla hajavaa mwili, tusome....                                         Yohana 1:1-3,14
       1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. 
14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. 
   *Kulingana na andiko hili tunaona kuwa:-
-Neno alikuwako wa Mungu
-Neno alikuwepo hapo mwanzoni, yaani hakuumbwa
-Neno ni Mungu
-Neno ni Yesu, kivipi? Msitari wa 14 - Neno alifanyika mwili akaja kukaa nasi hapa duniani kama mtu - YESU.
-Yesu ndiye Njia, Kweli na Uzima, ukitaka haya mambo matatu yapatikana kwa Yesu pekee na ndio maana wengine hutafuta usaidizi wa majini, Marohani, n.k ili wapewe msaada usio dumu.Hatuendi kokote bila Yesu, 
Soma,,, Yohana 14:6
       6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. 
Yohana 14:6
   - Hakuna mtume wala nabii yeyote aliyejitambulisha hivi kwa mamlaka aliyonayo isipokuwa Yesu, na ni katika kitabu takatifu pekee kiitwacho BIBILIA. Kama unamfuta na kumwabudu Yesu basi mjuate kikweli kweli na kumwabudu ibasavyo. Anasifa zote za kuabudiwa. Wote wamekufa bali Yesu Yu Hai mpaka sasa, kivipi? Matendo yake ya miujiza, ishara na Maajabu bado yanatendeka kwa jina lake, hakuna jina lingine litendalo hayo. 
Soma Matendo4:12......
    12  Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
  - Na ndio maana anatuita sote tuungane tumwabudu maana tuviumbe vyake. Zaburi 95:6-8
- Kuabudu Mungu halisia kunaambatana na Hofu ya Mungu, si kila mtu aliyeokoka ana hofu ya Mungu-mwenye hofu ya Mungu hutii kila kitu kihusianacho na Neno la Mungu. 
-Kuabudu binafsi kwafaa sana ila ni lazima kukusanyika na wengine siku za ibaada ya pamoja mfano jumapili, na siku za katikati,   (soma Waebrania 10:25) 
   25 wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia. 
-hilo ni agizo sio ombi, kuna wakati wa kufanya ibaada nyumbani, kifamiliya na kuna wakati wa kukusanyika na wengine ili kujifunza, kuonyana, n.k hebu fikiri ukiwa peke yako au na familiya yako ni nadra sana haya kufanyika kwa kukujenga ili umwabudu Mungu ipasavyo. 
-Kuwa na shughuli nyingi ni kuzuri sana ila muda wa Mungu apewe inavyotakikana. Kama ni shughuli basi Mungu yupo bize zaidi ya watu wote maana kila mnyama, mimea, binadamu wanamwitaji Mungu ili waendelee kuwepo, tafadhali tuchunge muda wa Mungu tusimwibie, tukikiuka hapa tunakuwa nje ya kusudi na lengo la kuumbwa kwetu. 
Tusipotambua aliyetuumba shetani hutumia nafasi hii kutubadilishia matumizi, na ndio maana kumekuwepo na Waabudu shetani, ma freemasonry na wengine wengi, huzuni sana hii. Tambua Muumba wako ili uwe salama, umwabudu Yeye akufikishe panapo stahili heshima.  
    TUTAENDELEA TENA NA SOMO HILI, Mungu azidi kukubariki unapozidi kufuatilia...... 


  






-👂👳👂👂👳👂👂

Chapisha Maoni

0 Maoni

Close Menu